Alhamisi 12 Februari 2026 - 01:00
Sherehe ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yafanyika nchini Armenia

Hawza/ Sherehe ya Mapinduzi kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu imefanyika katika mji wa Kapan nchini Armenia kwa ushiriki wa Wairani na Waarmenia wenye mapenzi kwa Imam na Mapinduzi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, hafla ya kumbukumbu ya miaka ya arobaini na saba ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ilizinduliwa tangu siku ya Jumamosi kwa kuandaliwa tamasha la bidhaa za mikono na bidhaa za Kiirani katika makao ya ubalozi mdogo (konsulati) wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mji wa Kapan, Armenia. Hafla hii tangu dakika za mwanzo ilipokelewa kwa shauku kubwa na wananchi wa Armenia, wafanyabiashara na Wairani wanaoishi Kapan.

Tamasha hili lililoandaliwa kwa mnasaba wa Siku za Mwenyezi Mungu za Muongo wa Alfajiri (Dahe-ye Fajr) ni ishara ya uhusiano wa kitamaduni na kisanaa kati ya nchi mbili jirani. Katika maonesho haya, kulikuwa na vibanda mbalimbali vya bidhaa halisi za mikono za Kiirani kama vile gilimu na verni, mapambo ya shaba, bidhaa za chakula na zawadi za Kiirani zilizooneshwa na kuuzwa.

Uwepo mkubwa wa wageni waliokuja kujifunza kuhusu utamaduni na ustaarabu wa Iran pamoja na kununua bidhaa za Kiirani ulijenga mazingira ya furaha na urafiki katika eneo la konsulati. Mapokezi haya yanaonesha mapenzi na uhusiano wa muda mrefu kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Kando ya maonesho hayo, pia ziliandaliwa programu za kitamaduni, ikiwemo kuoneshwa kwa klipu za makala za kumbukumbu (documentary) na maonesho ya picha kuhusu mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Tamasha hili lilianza shughuli zake siku ya Jumamosi na linaendelea hadi leo, na inatarajiwa kushuhudiwa ushiriki mkubwa zaidi wa wananchi wa Kapan katika tamasha hilo.

Inafaa kutajwa kwamba kuandaliwa kwa matukio kama haya katika mkoa wa Syunik kunachukuliwa kuwa hatua yenye athari katika kueleza maendeleo ya Iran baada ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuonesha urafiki kati ya nchi hizo mbili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha